JOSEPH MWEMEZI LUTA MKANDARASI WA BIOGAS.
MOB; +255-754393958, +255-686933838 +255-657878824Email: josephmwemeziluta@gmail.com
- Tunashughulika na ujenzi na ukarabati wa Mitambo ya Biogas tangu mwaka 1995 mpaka hivi sasa.
- Tunatoa mafunzo ya kujenga mitambo ya Biogas
MUHTASARI KUHUSU TEKNOLOJIA YA BIOGAS
Biogas ni mchamganyiko wa hewa ya ;
- Methene (CH4-60% VOL)
- Carbondioxide (Co2-36% VOL)
- Hydrogen (H)
- Hydrogen sulphide (H2C-0.3% VOL)
Mitambo inajengwa kwenye mashimo yaliyochimbwa kwa vipimo maalumu.
Vifaa
vinavyotumika kujengea ni tofari za kuchoma au block (ndogo) za kipimo
cha sm. 20×10×7, sementi, mchanga, kokoto, mawe, chokaa na water
proofer.


Njia ya gesi huunganishwa kwa kutumia bomba za chuma au plastic (Pu au IPS) za ukubwa wa ¾" na ½", kutoka kwenye mtambo hadi kwenye matumizi husika.
Baada ya ujenzi kukamilika kazi ya kujaza mtambo hufuatia. Kinyesi cha ng'ombe, nguruwe na kuku wa kwenye chanja (Cages), kinafaa zaidi. Unatumia uwiano wa 1:3 yaani ndoo moja ya kinyesi kwa ndoo tatu za maji/mkojo. Unakoroga na kutoa taka zote kisha unaingiza mchanganyiko huo kwenye mtambo kupitia kwenye bomba (inlate pipe). Zoezi la kulisha (kujaza) mtambo linakua endelevu kwa kadri unavyo tumia gesi.
Kwenye jumuia kubwa kama vile
Shule, Vyuo, Hospitali, Magereza n.k, tunatumia kinyesi cha binadamu
kwa kuunganisha moja kwa moja mashimo ya vyoo na mtambo wa biogas.
Mabaki
yaliyokwisha zalisha gesi husukumwa nje ya mtambo kupitia kwenye chemba
za kutolea (expansion chembers). Mabaki haya yanakua katika hali ya
ujiuji na hayana harufu, yanafaa kwa mbolea ya shambani na kwenye
bustani.
Mitambo inajengwa kwa ukubwa tofauti kulingana na mahitaji kama ifuatavyo:-
Mitambo inajengwa kwa ukubwa tofauti kulingana na mahitaji kama ifuatavyo:-
- Mitambo ya ukubwa wa 10m³, 12m³ na 16m³ (family size) Mitambo hii inafaa kwa famailia ya watu wa nne mpaka kumi. Unatakiwa uwe na ng'ombe wawili na kuendelea.
- Mtambo ya 30m³ (medium size) unafaa kwenye jumuiya ya watu 15 mpaka 30. Unatakiwa uwe na ng'ombe 6 na kuendelea.
- Mitambo ya 50m³, 75m³ na 100m³ (community plants) Mitambo hii ni mikubwa na inafaa kujengwa kwenye taasisi kubwa kama vile Shule, Vyuo, Hospitali, Magereza, na kwenye farm. Idadi ya ng'ombe ni 20 na kuendelea. Vile vile inaweza kutumia kinyesi cha binadamu.
Gharama za ujenzi zinategemeana na sehemu husika.
FAIDA ZA KUTUMIA MITAMBO YA BIOGAS.
- Kubana matumizi kwa kupata gesi ya kupikia, kuwashia taa, bunsen burner, fridge, Generator, mashine za kukuzia vifaranga (incubator).
- Kutunza mazingira kwa kupunguza matumizi ya kuni na mkaa.
- Kupata mbolea bora inayofaa kurutubisha ardhi.
- Biogas hailipuki kama gesi nyingine.
- Mitambo hii haiitaji ukarabati wa mara kwa mara.
- Mitambo inadumu kwa miaka 30 mpaka 40.
ANGALIZO!! Hatutengenezi mitambo kwa kutumia mapipa ya plastiki (SIMTANK)
Vilevile tunakarabati mitambo iliyojengwa chini ya kiwango kwa kuiboresha. Kama vile kuiwekea njia ya kukarabati ndani ya mtambo (neckset), kuiongezea uwezo wa kuzalisha gesi nyingi na kuhifadhi presha kwa muda mrefu n.k
Wasiliana nasi kwa mawasiliano yaliyopo hapo juu..
KARIBUNI.
Imetayarishwa na;
Joseph Mwemezi Luta
Mkandarasi na mratibu wa biogas
1995- 2024
1995- 2024


















































mbona hupokei cm
ReplyDelete