Wednesday, 6 March 2024

IJUE BIOGAS TANZANIA

JOSEPH MWEMEZI LUTA MKANDARASI WA BIOGAS.

MOB; +255-754393958, +255-686933838 +255-657878824
Email: josephmwemeziluta@gmail.com 

  • Tunashughulika na ujenzi na ukarabati  wa Mitambo ya Biogas tangu mwaka 1995 mpaka hivi sasa.
  • Tunatoa mafunzo ya kujenga mitambo ya Biogas 

MUHTASARI KUHUSU TEKNOLOJIA YA BIOGAS 

Biogas ni mchamganyiko wa hewa ya ;
  • Methene (CH4-60% VOL)
  • Carbondioxide (Co2-36% VOL)
  • Hydrogen (H)
  • Hydrogen sulphide (H2C-0.3% VOL)
Mchanganyiko huu wa gesi unatokana na taka zilizooza na kumeng'enywa na bacteria kwa muda wa takribani siku 30 hadi 90. Kazi hii hufanyika ndani ya mtambo wa biogas.

Mitambo inajengwa kwenye mashimo yaliyochimbwa kwa vipimo maalumu.
Vifaa vinavyotumika kujengea ni tofari za kuchoma au block (ndogo) za kipimo cha sm. 20×10×7, sementi, mchanga, kokoto, mawe, chokaa na water proofer.


Picha zifuatazo zinaonyesha hatua mbalimbali za ujenzi wa mitambo ya biogas.
                 




































               






Njia ya gesi huunganishwa kwa kutumia bomba za chuma au plastic (Pu au IPS) za ukubwa wa ¾" na ½", kutoka kwenye mtambo hadi kwenye matumizi husika.

Baada ya ujenzi kukamilika kazi ya kujaza mtambo hufuatia. Kinyesi cha ng'ombe, nguruwe na kuku wa kwenye chanja (Cages), kinafaa zaidi. Unatumia uwiano wa 1:3 yaani ndoo moja ya kinyesi kwa ndoo tatu za maji/mkojo. Unakoroga na kutoa taka zote kisha unaingiza mchanganyiko huo kwenye mtambo kupitia kwenye bomba (inlate pipe). Zoezi la kulisha (kujaza) mtambo linakua endelevu kwa kadri unavyo tumia gesi.
Kwenye jumuia kubwa kama vile Shule, Vyuo, Hospitali, Magereza n.k, tunatumia kinyesi cha binadamu kwa kuunganisha moja kwa moja mashimo ya vyoo na mtambo wa biogas. 
Mabaki yaliyokwisha zalisha gesi husukumwa nje ya mtambo kupitia kwenye chemba za kutolea (expansion chembers). Mabaki haya yanakua katika hali ya ujiuji na hayana harufu, yanafaa kwa mbolea ya shambani na kwenye bustani.

Mitambo inajengwa kwa ukubwa tofauti kulingana na mahitaji kama ifuatavyo:-
  1. Mitambo ya ukubwa wa 10m³, 12m³ na 16m³ (family size) Mitambo hii inafaa kwa famailia ya watu wa nne mpaka kumi. Unatakiwa uwe na ng'ombe wawili na kuendelea.
  2. Mtambo ya 30m³ (medium size) unafaa kwenye jumuiya ya watu 15 mpaka 30. Unatakiwa uwe na ng'ombe 6 na kuendelea.
  3. Mitambo ya 50m³, 75m³ na 100m³ (community plants) Mitambo hii ni mikubwa na inafaa kujengwa kwenye taasisi kubwa kama vile  Shule, Vyuo, Hospitali,  Magereza, na kwenye farm. Idadi ya ng'ombe ni 20 na kuendelea. Vile vile inaweza kutumia kinyesi cha binadamu.

Gharama za ujenzi zinategemeana na sehemu husika. 

 FAIDA ZA KUTUMIA MITAMBO YA BIOGAS.

  1. Kubana matumizi kwa kupata gesi ya kupikia, kuwashia taa, bunsen burner, fridge, Generator, mashine za kukuzia vifaranga (incubator).
  2. Kutunza mazingira kwa kupunguza matumizi ya kuni na mkaa.
  3. Kupata mbolea bora inayofaa kurutubisha ardhi.
  4. Biogas hailipuki kama gesi nyingine.
  5. Mitambo hii haiitaji ukarabati wa mara kwa mara.
  6. Mitambo inadumu  kwa miaka 30 mpaka 40.
ANGALIZO!! Hatutengenezi mitambo kwa kutumia mapipa ya plastiki (SIMTANK)
         Baadhi  ya vifaa na matumizi ya biogas.



























 Vilevile tunakarabati mitambo iliyojengwa chini ya kiwango kwa kuiboresha. Kama vile kuiwekea njia ya kukarabati ndani ya mtambo (neckset), kuiongezea uwezo wa kuzalisha gesi nyingi na kuhifadhi presha kwa muda mrefu n.k

 Wasiliana nasi kwa mawasiliano yaliyopo hapo juu..
                      
                                                               KARIBUNI. 
                                                       Imetayarishwa na;
                                                    Joseph Mwemezi Luta 
                                          Mkandarasi na mratibu wa biogas
                                                               1995- 2024